HOPE SERVICE STATION

nsekwa

RJ COMPUTER IRINGA

GARIIIIIIII

ALTEZA

highlanda

RJ

IBS Inc


bravoooo

April 23, 2014

HOT News GARI DOGO AINA YA TAXI YAGONGA LORI NA KUPELEKEA LORI HILO KUPINDUKA IRINGA

Hili ndilo lori lenye namba T 388 BHA  lililogongana na Taxi eneo la Gangilonga mjini Iringa
Hili ndilo Taxi lenye namba  T 976 AYD ambalo limegongana na lori
Mashuhuda  wakishangaa maajabu hayo
Hili ndilo gari dogo aina ya Taxi iliyoligonga  lori na kupinduka huku lenyewe likiwa ngangari
askai wa  usalama  barabara  mjini Iringa  wakilitazama  lori  lililogongwa na Taxi mali ya kampuni ya Papu na kupelekea  kupinduka kwa lori  hilo

Mashuhuda wa  tukio   hilo  waliueleza mtandao huu wa  www.matukiodaima.com kuwa   TXi hiyo  ilikuwa ikiingia barabara  kuu bila  kusimama kama sheria  inavyotaka na kuligonga  lori  lililokuwa  likitoka  eneo la Ikulu  kuelekea mjini  hadi kupelekea lori hilo  kupinduka  huku Taxi hiyo ikisamilika  zaidi ya kupitiwa upande wa  mbele  katika eneo la boneti .

Mbali ya  kushangaa tukio hilo  ila bado wamedai kuwa  kuna haja ya askari wa usalama  barabara  kumbana pia dereva wa  lori  kwani ni jambo la kushangaza ambapo eneo  hilo la mjini sheria inataka  magari kutembea  mwendo wa mdogo kati ya spidi  30 hadi 50  iweje  lori hilo  lipite kwa mwendo kasi .
Kwani  walisema  kuwa iwapo  lori hilo  lingekuwa  katika mwendo wa kawaida  lisinge  gongwa na taxi hiyo hadi kupinduka  .

Katika  tukio hilo  hakuna mtu aliyejeruhiwa  zaidi ya magari hayo mawili kuharibika  vibaya na kuwa  tukio hilo limetokea mida ya saa 1.10 usiku huu .

TAARIFA:MH:MWIGULU NCHEMBA KUONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA JMT NCHINI MAREKANI-WASHINGTON DC

 MG 9209 b0822TAARIFA KWA UMMA
Naibu Waziri wa Fedha(S) Mh:Mwigulu Lameck Nchemba(Mb) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Tanzania Bara ataongoza Sherehe za Kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania Kwa Watanzania Waishio Nchini Marekani-Washington-DC na Viunga Vyake.
Maadhimisho hayo yanayotegemewa Kufanyika Tar.26/04/2014 katika Ukumbi wa MATINICE EVENTS AND CONFERENCE CENTRE,7925 CENTRAL AVE,CAPITOL HEIGHTS,MD 20743.
Mh:Mwigulu Nchemba aliyealikwa na Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Mh:Libereta Mulamula kuongoza Sherehe hizo za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano,atazungumza na Watanzania kuhusu Muungano Wetu,Kuulinda,Kuutetea na Kuudumisha kwa Manufaa ya Taifa letu la Tanzania na Watu Wake.
Watanzania Wote Mnaombwa Kufika kwa Wingi kwenye Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhai wa Muungano Wetu,Hii ni nafasi nzuri kwa Watanzania Nchini Marekani kuandika Historia Mpya kwa Taifa letu.
Mungu Ubariki Muungano Wa Tanzania,
Mungu Ibariki Tanzania.
Imetolewa na
Ofisi ya Naibu Waziri wa Fedha(S)
Mawasiliano.
23/04/2014

WAZIRI GHASIA AONGOZA MAZISHI YA DC MOSHI CHANG'A , SPIKA MAKINDA AMLILIA ASEMA NDIE ALIYEMNUSURU KUANGUSHWA NA NCCR MAGEUZI JIMBONI NJOMBE KUSINI 1995

Utaratibu  wa mazishi  ukiwekwa
DC Mwamoto kulia na DC Warioba  wakiwa msibani hapo
DC Mwamoto akiweka  sahii kitabu cha maombolezo  leo
Spika Makinda akitoa  mkono wa pore kwa wafiwa
Spika Makinda  kulia akimpa pore waziri Hawa Ghasia
Spika Makinda  akiwapa pore  wafiwa
Spika  wa bunge Anne Makinda akiwa amepiga magoti  kuwapa  pole  wafiwa katika msiba wa aliyekuwa DC wa kalambo Moshi Chang'a leo mjini Iringa
Waombolezaji  wakiwa katika msiba  huo  leo
Spika wa bunge Anne makinda akisaini kitabu cha maombolezo ya DC Chang'a leo
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia akisaini kitabu  cha maombolezoo ya  aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Mussa Chang'a leo nyumbani kwake mjini Iringa kabla ya mazishi  yaliyofanyika makaburi ya Mtwivila 
Spika Anne Makinda akiteta  jambo na waziri Hawa Ghasia  leo
Mwanahabari  Eliasa Ally Chang'a( kulia)  ambae ni ndugu na DC Chang'a akiwa na waombolezaji  wengine Msafiri Mtandi kushoto na Said kalinga katikati
Mwenyekiti  wa CCM Kilolo Sety Mwamoto kulia  akiwa na mdau
mfanyabiashara  mkubwa Iringa Pilly MOhamed  akisainia kitabu cha maombolezo
Mkuu wa mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma akisaini kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya kalambo Rukwa marehemu Moshi  Chang'a wanaoshuhudia ni mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita kushoto na mkuu wa wilaya ya  Iringa Dr Leticia Warioba katikati ,hapa ni nyumbani kwa marehemu eneo la Kihesa mjini Iringa
RC Mbeya Bw kandoro  akiwapa pore  wafiwa
Mke wa mkuu wa mkoa wa Mbeya akisaini kitambu cha maombolezo ya Dc Chang'a
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro  akiweka sahihi katika  kitabu cha maombolezo  leo
Waombolezaji  na ndugu  wakiwa katika viwanja vya maombolezo  leo
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza akitoa  salam za chama
Kiponza akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro  leo
Mbunge Msigwa akiwa na mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akitoa  salama zake na za Chadema pamoja na ubani wa TSh 100,000
Vijana  wa  CCM wakiweka mambo  sawa
Wakuu wa  wilaya  mbali mbali nchini  wakiwa  wameubeba mwili wa DC mwenzao Moshi Chang'a leo
Mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamwoto  kulia akishirikiana na mkuu wa wilaya ya Mwanza  kukunja bendera  iliyotumika kufunika mwili wa DC Chang'a
Kada wa CCM Iringa mjini Frederick Mwakalebela akishiriki msiba  huo
Wakuu wa wilaya na wananchi  Iringa  wakiwa  wamebeba mwili wa Dc Chang'a mjini Iringa leo
Waombolezaji  wakiwa  wameubeba mwili  huo
Mwili wa DC Chang'a ukipelekwa msikiti wa Mwanchang'a Kihesa
Waombolezaji  wakielekea msikitini  leo
Umati wa wananchi  wakielekea makaburi ya Mtwivila  leo
Msafara  wa kutoka nyumbani kwa DC Chang'a kwenda msikitini
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi kushoto akifuatilia kwa karibu mazishi ya DC Chang'a leo
msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete katika masuala ya siasa Ikulu Rajab Luhwavi kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita kulia  wakati wakielekea kumzika Dc Chang'a leo mjini Iringa .
 
WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia leo  amemwakilisha  waziri  mkuu Mizengo Pinda katika mazishi  ya  aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Marehemu Moshi Chang'a.

Katika mazishi  hayo yalihudhuriwa na mamia  ya  wakazi  wa Manispaa ya  Iringa na viongozi  wa serikali  kutoka mikoa mikoa  mbali mbali nchini pia  spika  wa  bunge Anne Makinda  alitumia nafasi hiyo  kuueleza  umma siri  nzito  iliyofichika  dhidi yake ya marehemu Chang'a mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza  ulioshirikisha vyama  vingi kuwa bila marehemu huyo asingeweza kuwa mbunge kutokana na kubanwa na chama cha upinzani cha NCCR Mageuzi kwa  kipindi  hicho

"Mimi  nimekuwa kwa niaba yangu mwenyewe na  jimbo la Njombe  kusini ambalo mimi ni mbunge  wake ....mwaka  1995 marehemu  alikuwa ni katibu  wa CCM Njombe na ndio mwaka  ambao  mfumo wa vyama  vingi  ulianza na yeye ndie  alikuwa katibu  na jimbo hilo  upinzani  ulilizingira kweli na hata kwa kukanyanga mguu kulikuwa hakuna  ila bila Chang'a kweli jimbo  hilo   niseme ukweli  lingekuwa limechukuliwa na Upinzani na kwa kipindi hicho chama chenye nguvu zaidi  kilikuwa ni NCCR Mageuzi "

Akizungumza   wakati wa kutoa  salama  mbali mbali kwa  viongozi  mjini  Iringa Spika Makinda  alisema  kuwa kwa mara ya kwanza  mwaka 1995  alibanwa kupita  kiasi na  NCCR Mageuzi  katika jimbo lake la uchaguzi la Njombe kusini na  kuwa  bila marehemu  huyo ambae kwa kipindi  hicho alikuwa ni katibu wa CCM wilaya ya Njombe kamwe asingeweza kuwa mbunge .

Mkuu wa  mkoa  wa Rukwa injinia Stella Manyanya  alisema kuwa  mkoa  wake amempoteza  kiongozi mzalendo na aliyependa kazi yake na kuwa hata  akiwa  safarini hakuwa na shaka na utendaji kazi wa mkuu  huyo wa  wilaya na kuwa  siku  zote mbali ya kuongoza kama kiongozi wa serikali ila wakati mwingi alitumia  kuwahubiria upendo  wananchi wa  wilaya  yake.

Kwani  alisema kuwa alikuwa hawezi kuanza mkutano  bila kumhubiri  mwenyezi Mungu mbali ya kuwa  yeye alikuwa muumini wa dini ya Kiislam ila alikuwa akihubiria dini ya kikristo  .

Hata  hivyo  alisema kuwa  hadi  kesho anaamini  alishinda  ubunge  jimbo hilo mwaka 1995 si kwa uwezo wake  bali  alishinda kwa uwezo wa marehemu Chang'a ambao  alionyesha  uwezo mkubwa  wa kumnadi na hata kufanikiwa  kuwa mbunge wa  jimbo hilo na leo  kuwa  spika wa bunge .

Alisema  iwapo  angekwama  kuwa  mbunge  mwaka 1995  basi yawezekana leo asingekuwa spika kwani angekuwa amekata tamaa ama angekuwa mbunge  mwingine katika jimbo hilo.

Aidha  alisema mbali ya  kushinda  ubunge  wake bado  wapinzani  walikwenda mahakamani kupinga matokea  ila Chang'a alisimama   na makada  wenzake  wawili moja akiwa ni marehemu  sasa katika kumtetea mahakamani kwa miaka  minne  yote na mbali ya hujuma  kubwa zilizokuwa zikifanywa na Halmashauri ya Njombe kwa kuharibu  baadhi ya nyaraka  za ushahidi ili kuwawezesha NCCR Mageuzi kushinda kesi hiyo japo kwa Chang'a walishindwa kutokana na kuwa na nyaraka  hizo kwa mwenendo mzima wa mchakato  wa uchaguzi huo hadi mahakama  ilipompatia ushindi yeye kama mbunge halali wa jimbo hilo.

" Leo nafanya kazi hii ya uspika kwa kuwa Chang'a ndie  aliyeniweka hapa na bila  yeye  kujituma  mimi  nisingesimama hapa kama spika ....jamani nasema  tuendelee  kujituma katika kazi zetu kama alivyofanya marehemu Chang'a nasema kila mmoja atapimwa utendaji kazi wake hapa duniani "

Kwa  upande  wake  mkuu wa  mkoa wa Mbeya  Abas Kandoro  akimuelezea  Chang'a wakati wa kutoa  salam  hizo  alisema  kuwa  kamwe  hata  sahau utendaji kazi wa mkuu  huyo wa wilaya  ambae amepata  kufanya nae kazi katika wilaya ya Makete ambapo  yeye akiwa mkurugenzi Chang'a alikuwa ni kiongozi wa  CCM wilaya  hiyo  na baada ya kwenda Mbeya  pia  Chang'a amefanya kazi kama mkuu wa wilaya katika mkoa  huo  .

Kandoro alisema kuwa  utendaji  kazi na utumishi  uliotukuka wa  Chang'a ni mfano  wa  kuigwa kwa watumishi wengine wa umma katika Taifa  hili.

Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma  alisema kuwa mkoa  wa Iringa  umepata  pigo kubwa kwa  kifo cha mkuu  huyo wa wilaya  hasa ukizingatia mchango mkubwa wa kimaendeleo ambao amepata  kuonyesha ndani ya mkoa na nje ya mkoa na kuwa kamwe  mkoa  utaenzi yote aliyoyaacha .

Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa  alisema kuwa  wananchi wa Manispaa ya Iringa na mkoa  wa Iringa  tumeendelea  kupoteza  wakuu wa wilaya na kuwa mbali ya Chang'a pia  tumepata  kumpoteza mkuu wa wilaya ya Tabora  na kuwa viongozi hao  wote ni pengo kubwa kwa Taifa .

Mbunge Msigwa alisema kuwa akiwa kama mbunge wa jimbo hilo la Iringa mjini na kiongozi wa Chadema  wilaya  hiyo amepokea kwa masikitiko kifo hicho na kuwa sote kama viongozi  tunapaswa kuangalia ni barua gani ambayo inaachwa kwa jamii baada ya kuondoka na kuwa Chang'a alikuwa ni kiongozi asiyependa  kumchukia mtu na  kila wakati alikuwa ni mtu wa kucheka na kila mmoja.

Awali  akiwasilisha  salama  za  serikali waziri  Ghasia  alisema kuwa  kifo  hicho  kimeacha pengo  kubwa na kumtaja marehemu Chang'a katika mkuu wa wilaya wa mfano  ambae hakupenda  kukataa wala kuonyesha kupinga kwa sehemu  yeyote anayopangiwa kwenda kuwakilisha  wananchi .

Viongozi  wengine  waliopata  kushiriki katika mazishi hayo ni pamoja na viongozi  msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete katika masuala ya siasa Ikulu Rajab Luhwavi pia viongozi kutoka mkoa wa Mwanza , Singida ,wabunge  wa bunge la jamhuri ya muungano  akiwemo mbunge wa  viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati na Lediana Mafulu (CCM) naibu  waziri wa maliasili na utalii Mahamudu Mgimwa ambae  pia ni mbunge wa  jimbo la Mufindi kaskazin,baadhi ya  wajumbe wa bunge la katiba  kutoka mkoa  wa Iringa na wakuu wa wilaya mbali mbali akiwemo mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamwoto mkuu wa  wilaya ya Iringa Dr Letisia Warioba ,mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita  na wengine  wengi
VIDEO  YA  MAZISHI ITAKUJIA MAPEMA  KESHO