HOPE SERVICE STATION

nsekwa

RJ COMPUTER IRINGA

GARIIIIIIII

ALTEZA

highlanda

RJ

bravoooo

April 21, 2011

WANA CCM WAFUNGUKA SASA WATAKA KILA JAMBO LIWE KWA MAANDISHI, WAZEE NA MAFISADI WAAMBIWA WAKAA NJE...


Kada wa CCM mzee Byemelwa (kushoto) akimpasulia jibu Nape juu ya sababu ya CCM kuendelea kudoda
Kada wa CCM Byemelwa akipongezwa na Nape kwa kusema ukweli kuhusu ubovu wa CCM
Makada wa CCM Iringa wakimpokea katibu wa itikadi na uenezi CCM Taifa Nape Nnauye
Naibu katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Bara John Chiligati (wa tatu kushoto) na katibu wa itikadi na uenezi Taifa Nape Nnauye akiwa na viongozi na wanachama wa CCM mkoa wa Iringa baada ya kumaliza mkutano wa hadhara kwa ajili ya opresheni ya Vua gamba uliofanyika mjini Iringa
mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa mjini Bw.Ibrahim Ngwada (kulia) akiwa na madaka wengine wa CCM wakimsikiliza naibu katibu mkuu


wana CCM wakimsikiliza naibu katibu mkuu kwa umakini zaidi

Naibu katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) Bara John Chiligati(katikati mwenye kofia) akiwa na viongozi wa CCM mkoa wa Iringa wa pili kushoto ni kamanda wa umoja wa vijana mkoa wa Iringa Salim Abir Asas na kulia ni katibu wa CCM mkoa wa Iringa mary Tesha
Baadhi ya wanachama wapya wa CCM ambao wametokea vyama vya upinzani wakila kiapo mbele ya naibu katibu mkuu
wanachama wa CCM mkoa wa Iringa wakionyesha mikono juu kuungana na wanachama wapya kula kiapo
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa vijijini Delophina Mtafilalo ,kamanda wa UVCCM mkoa wa Iringa Salim Asas na mbunge wa jimbo la Kalenga Dr.Wiliam Mgimwa wakiungana na wanachama wapya kula kiapo.

HUKU viongozi wapya wa Chama chama cha mapinduzi (CCM) wakizunguka mikoani kueleza juu ya gamba lililovuliwa Dodoma na kuwatuliza wana CCM ambao walikuwa wakiendelea kuondoa imani yao CCM kutokana na mafisadi kukichafua chama hicho ,wana CCM mkoani Iringa juzi waligeuka mbogo mbele ya naibu katibu mkuu CCM bara John Chiligati na katibu wa itikadi na uenezi Taifa Nape Nauye wakiwataka kuchukua maamuzi mazito ya kuwafukuza mafisadi hao ndani ya chama na wali waliopo serikalini kuwawajibisha pamoja na kuwaegua wazee wote katika nafasi za juu ya chama.

Pia wana CCM wawdai wamechoshwa kugeuzwa mbumbumbu na kutaka maamuzi ya kujivua gamba na yale ya kuwaandikia barua mafisadi ili kujiondoa wenyewe CCM na serikali yafanyike kwa maandishi na nakala zake kusambazwa kwa wanachama ili wakiendelea kuwepo mara baada ya muda kumalizika basi magamba mapya yaliyowekwa kubadili ya zamani kuvuliwa pia.

Hatua hiyo ilijitokeza baada ya katibu wa CCM mkoa wa Iringa Mary Tesha kumtaka mwenyekiti mstaafu wa CCM wilaya ya Iringa mjini mzee Andwer Byemelwa kupanda jukwaani kushukuru hotuba ya naibu katibu mkuu kwa niaba ya wanachama wengine waliofika katika viwanja vya CCM mkoa kuwapokea na kuwasikiliza viongozi hao.

Kada huyo wa CCM alisema suala la kuvua gamba ni sawa na mchezo wa kuigiza iwapo CCM itaendelea kuwakumbuatia waliokifikisha chama hapa kilipo ambapo ni pabaya zaidi .

Kwani alisema kuwa uongozi wa CCM Taifa ndio uliohusika kukivuruga chama hicho kwa kuwakumbatia mafisadi ambao wameendelea kuharibu chama bila kuwajibishwa zaidi ya viongozi hao kurudi tena kwa wananchi na kudai wamevua gamba huku wakiendelea kuwaacha waliovuliwa ndani ya chama.

Alisema kuwa itapendezwa gamba la CCM kuanza kutua kwa viongozi wa mikoa ,wilaya na mashina ambao walivalishwa gamba la ufisadi na m afisadi waliopo juu huku watendaji wabovu serikalini wakiwajibika haraka badala ya kuacha gamba hilo kujijenga upande wa pili.

Pia alisema kuwa CCM itaendelea kudumu iwapo viongozi wote wazee ndani ya chama wakaenguliwa na kuwaachia vijana wenye sifa kukiogoza chama hicho .

"Hatuna hata mmoja aliyezaliwa na kuambiwa kuwa wewe utakuwa Rais wa Tanzania ila vitendo vyake ndivyo vinavyoonyesha kuwa na sifa ya kutawala hivyo CCM isiendelee kuwalazimisha wananchi kuwachagua kwa nguvu wazee ambao hawana sifa ya uongozi na badala yake wazee sasa kukaa pembeni na kuwaachia vijana waongoze nchi....tunataka sasa kila mnachosema kiwe kwa maandishi ili mkienda kinyume tuweze kuwawajibisha kwa ushahidi zaidi...wana CCM wa leo sio wale wa mwaka 1960 sasa wasomi ni wengi na vijana wapo tuwape nafasi tusione haya kuonea haya katika hili ..kwinini na chungu ila mgonjwa ukimnywesha kwa mguvu akipona atakushuruku hivyo lazima tutumia maamuzi magumu kukinusuru chama chetu ...wahenge walisema mficha maradhi kifo kitamuumbua"

Kwa upande wake Chiligati alisema kuwa baada ya mageuzi ya Dodoma sasa CCM imekuwa ni mpya ambapo kamwe haita kubali mafisadi kuendelea kuwepo ndani ya chama hicho kipya na kuwa kwa sasa wote watapewa barua za kujiondoa wenyewe CCM na kama watashindwa kufanya hivyo wataondolewa kwa aibu ikiwa ni pamoja na kufukuzwa hadharani.

"Mzee Byeleywa amesema mbona majina mmefunga funga....sasa nasema hivi kwa sasa tunafanya kuwalindia heshima kama wasipo kubali kulindiwa heshima basi tutawaondoa kwa aibu....suala la wazee kuondoka tunalifanyia kazi na kubwa vijana zingatieni elimu ili kuweza kuwaondowa wasio na sifa"

Pia alisema kuwa makosa ambayo CCM iliyafanya kwa kumuengua mshindi wa kura za maoni katika jimbo la Iringa mjini kamwe hayatarudiwa tena na kuwa sasa NEC ya Taifa iliyokuwa ikifanya kazi ya kuchuja wagombea sasa imerudishwa ngazi ya vitongoji ambao wana CCM wenyewe ndio watachuja wagombea na sio vikao vya mjini Dodoma tena.

Chiligati alisema kuwa CCM ya mwanzo ilikuwa ni ya wanyoge na wakulima ila sasa hivi iligeuka kuwa ya matajiri na mafisadi wachache ambao walkiendelea kukivuruga chama hicho na kufanya wananchi kukichukia na kuwa makosa hayo kamwe hayatajirudia tena na sasa CCM kitakuwa ni chama kama cha zamani enzi za mwalimu.


Pia Chiligati alisema ni aibu kwa Halmashuuri za wilaya kupata hati chafu huku viongozi wa CCM wapo na kuwa Halmashauri zilizofanya vibaya kujitathimini na kama mafisadi walijipenyeza basi waanze kujiengua.


Huku katibu wa itikadi ya uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Nape Mnauye amegeuka mbogo mkoani Iringa kwa kudai kutaka moto ulioanzishwa na mwenyekiti wa chama hicho Taifa Rais Jakaya Kikwete kwa kuwavua magaba mafisadi waliokuwa wakivuraga chama hicho kugeukia kwa viongozi wa serikali.

Nape ambaye katika ziara yake ya Opresheni ya Vua Magamba mkoani Iringa aliambatana na naibu katibu mkuu huyo Taifa Chiligati pia alipokea wanachama 80 wa chama cha NCCR Mageuzi .

Alisema kuwa moto liowasha Dodoma kwa kuwaegua vionozi waliokuwa wakivuruga chama hicho ni moto ambao unaanza kushushwa nazi ya chini za CCM na serikali yake na kuwa kwa sasa kama yupo kiongozi ambaye wananchi wanamjua kama ni fisadi basi wamtaje ili katika opration ya vua gamba serikalini kuvuliwa rasmi.

"Tunajua kuwa hata hapa jimbo la Iringa mjini CCM imelipoteza kutokana na kuwepo kwa viongozi wasaliti ambao walikwa wakiendekeza ufisadi na kusahau kuwatumikia wananchi ....sasa tunasema kuwa wakati umefika kwa wana CCM mafisadi na watendaji wa serikali mafisadi kujiengua wenyewe...hatutakubali serikali kuendelea kuchafuliwa na mafisadi wachache wasiopenda kuwajibika"

Pia alisema kuwa CCM wapo wanaosema kuwa moto wake ni kwa ajili ya kuingia katika mchakato wa mbio za Urais mwaka 2015 jambo ambalo halina ukweli na kuwa umri wake haumruhusu kugombea Urais .

Nape pia aliwataka wanaomvuruga Rais Kikwete na kumhusisha na tuhuma za ufisadi kuacha mara moja na kuwa iwapo Rais Kikwete angekuwa ni fisadi na tatizo basi asingekubali kuwavua magamba wenzake .

1 comment:

Anonymous said...

CCM wanajigamba wamewafanyia nini wananchi wa mkoa wa Iringa? Baada ya Uhuru wilaya nyingi za mkoa wa Iringa hazijaunganishwa na rami kutoka wilaya moja kwenda ingine. Nenda Ludewa, Makete, Kilolo n.k tunataka maendeleo sio shamla shamla hizo ambazo wanao nufaika ni viongozi wa CCM na wachache wenye uelewa mdogo ambao wananufaika ugua pole ya kofia, khanga, na flana.

Post a Comment

KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA