Pamoja na ufaulu huo jumla ya wanafunzi 737 waliofanya mtihani huo mwaka huu wamefutiwa matokeo yao kutokana na kufanya udanganyifu katika ufanyaji wa mitihani hiyo.
Kutokana na hali hiyo Serikali mkoani Iringa imezipongeza Halmashauri za wilaya ya Kilolo na Iringa vijijini kwa kufanikisha kupiga hatua katika ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba .
Mwenyekiti wa kikao cha uteuzi wa wanafunzi waliofaulu mkoa wa Iringa katibu tawala wa mkoa Getrude Mpaka alisema kuwa ufaulu wa wanafunzi hao ni changamoto kubwa kwa wilaya kuongeza idadi ya vyumba vya madarasa pamoja na kuongeza madawati zaidi.
Alisema kuwa mkoa wa Iringa unaongoza kwa kuwa na misitu mingi ya mbao hivyo ni aibu kuona shule zinakabiliwa na uhaba wa madawati..
I...........naendelea endelea kubaki katika mtandao.............
1 comment:
sasa mbona hujatupa tasmini ni Mkoa gani umekuwa wa kwanza nani kawa mwanafunzi bora?tupe mainfo mkuu
Post a Comment