Habari za kusikitisha zilizotua hivi punde katika mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka mkoani Arusha zinadai kuwa msanii maarufu aliyejizolea umaarufu kwa kibao chake cha Mimi Mmasai Bwana Mr Ebo amefariki dunia mapema leo Mwandishi wa mtandao huu kutoka Arusha John Samwel anaripoti kuwa kifo cha msanii huyo kimeacha simanzi kubwa kwa wananchi wa mkoa wa Arusha .
Imedaiwa kuwa Msanii huyo alikuwa akisumbuliwa na homa kwa muda mrefu na kutibiwa katika Hospital mbali mbali hapa nchini na nje ya nchi na baada ya hapo aliamua kupata matibabu ya dawa za kienyeji akiwa nyumbani kwake .
Taarifa zaidi juu ya kifo cha msanii huyo utaendelea kuzipata katika mtandao huu.
2 comments:
RIP MR EBO HAKIKA WATANZANIA TUNATAMBUA MCHANGO WAKO KATIKA TASNIA YA MUZIKI
Kifo cha Mr . Ebo sio pigo kwa watanzania tu mbali ni kwa watu wa Africa mashariki na wapenzi wa nyimbo zake ulimwenguni.
Nderitu wa laikipia county, Kenya.
Post a Comment