HUKU mkoa wa Iringa ukiwa umepewa hadhi ya kuwa mwenyeji wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani kwa mwaka huu ,mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinda ashuhudia ajali mbaya iliyopelekea vifo vya watu wanne kufa papo hapo na mmoja kujeruhiwa vibaya baada ya malori mawili kugongana na kutumbukia bondeni katika mteremko wa mlima kitonga wilayani Kilolo katika barabara kuu ya Iringa - Dar es Salaam .
Hata hivyo dereva wa lori bovu ambalo lilikuwa limeegeshwa eneo hilo alipona katika ajali hiyo .
Akizungumza katika eneo la ajali mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Taifa Mohamed Mpinga alisema kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia jana na kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori lenye namba za usajili T587 BGP aina la scania ambalo lilikuwa na mali mbali mbali za dukani lilikuwa limeharibika na kuegeshwa kando ya barabara hiyo kugongwa na lori lenye namba za usajili T T319 BDG aina ya Scania ambalo lilikuwa limebeba shaba kuligonga lori lililokuwa limeegesha kando ya barabara hiyo.
Mpinga alisema kuwa katika ajali hiyo watu wanne walikufa papo hapo na mmoja ambaye ni kijana alijeruhiwa vibaya na kuwa miongoni mwa waliokufa ni pamoja na mwanamke mmoja ambaye inasadikika ni mkazi wa wilaya ya kilolo aliyekuwa amepanda katika lori hilo .
Alisema kuwa miongoni mwa waliopoteza maisha ni pamoja na utingo wa lori ambalo lilikuwa limeegeshwa kando ya barabara hiyo ambalo lilikuwa limebeba mali za dukani ambaye alikuwa nje ya lori hilo akifanya mawasiliano ya simu na mwenzake na hivyo kugongwa na lori hilo la Shaba ambalo breck zilionyesha kuwa na matatizo.
Hata hivyo alisema kuwa pamoja na ajali hiyo kutokea Agosti 4 majira ya jioni ila zoezi la utoaji wa maiti ya dereva wa lori hilo lenye shaba bado ni gumu kutokana na mwili wa dereva huyo kubanwa vibaya ya tela la lori hilo lenye shaba .
Alisema kuwa kabla ya tela hilo lenye shaba kufunika kibini ya lori hilo kebini hiyo ilikatika na kutangulia korongoni na baada ya hapo tela lenye shaba kufuata nyuma na kutua juu ya kibini hiyo.
kamanda huyo alisema kuwa ajali hiyo imetokea wakati mkoa wa Iringa unataraji kuwa mwenyeji wa wiki ya nenda kwa usalama ambayo kitaifa itafanyika katika mkoa wa Iringa huku akiwataka madereva kuheshimu sheria za usalama barabarani kama njia ya kuepuka ajali kama hizo.
Aidha alisema kuwa kutokana na eneo hilo la mlima wa Kitonga kuendelea kuwa na eneo maarufu kwa ajili tayari mkakati umewekwa kwa ajili ya kuongeza ulinzi en eo hilo pamoja na kufanya doria za mara kwa mara za miguu ya magari kwa askari wa usalama barabarani ili kusaidia kupunguza ajali katika eneo hilo.
Alisema kuanzia sasa askari wa usalama barabara watawekwa eneo hilo ili kuweza kukagua magari yote ya abiria na mizigo ili kabla ya kushuka mteremko huo kuwa na uhakika wa breck kama njia ya kuanza kuchukua hatua za kukabiliana na ajali mbaya katika mteremko huo.
No comments:
Post a Comment