WAKATI maandalizi ya sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika usiku wa Agosti 25 kuamkia Agosti 26 mwaka huu yakiendelea kuchukua kasi hapa nchini , mkuu wa mkoa (RC) wa Iringa Dkt Christine Ishengoma amepiga marufuku viongozi kuwa kuwasumbua wananchi kwa michango kwa kipindi hiki cha kuelekea katika zoezi la Sensa ya watu na
makazi.
Pia atangaza kumchukulia hatua kali ya kisheria kiongozi yeyote ambaye
atabainika kuomba fedha kutoka kwa wananchi pindi anapokuwa katika
majukumu yake ya kuhamasisha zoezi la sensa .
Dkt Ishengoma alitoa agizo hilo leo alipozungumza na mwandishi wa
habari hizi ofisini kwake na kudai kuwa ili kufanikisha zoezi hilo la
Sensa ya watu na makazi katika mkoa wa Iringa amelazimika kusimamisha
michango yote ya maendeleo kwa wananchi ili kuwaondoa na hofu mbali mbali juu
ya michango hiyo na badala yake kujiandaa kwa kuhesabiwa pekee.
Hatua ya mkuu huyo wa mkoa wa Iringa kupiga marufuku viongozi
kuchangisha wananchi michango mbali mbali ya kimaendeleo imekuja baada ya
kuibuka kwa vitendo vya baadhi ya viongozi kuidaiwa kupita kwa wananchi
na kukusanya michango ya maendeleo huku baadhi ya wananchi wakianza
kuingiwa na hofu kuwa yawezekana viongozi hao wakatumia siku hiyo ya sensa
kuwakamata kwa kushindwa kulipa michango.
Alisema kuwa ni vema kwa kipindi hiki cha kuelekea katika zoezi hilo
la sensa viongozi wa vijiji,mitaa kata na wilaya kuachana na mpango wa
kupita kwa wananchi kuchangisha michango hiyo ama kuhamasisha juu ya
wananchi kuchangia miradi ya maendeleo ili kuwafanya wananchi hao kujiandaa
kwa kuhesabiwa pekee.
Dkt Ishengoma alisema kuwa kazi kubwa ambayo viongozi wote
wanapaswa kuifanya kwa sasa ni kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa
badala ya kuwatisha kwa michango ya maendeleo.
Alisema kuwa michango ambayo wananchi wanaweza kuendelea kuchangia ni
ile ya kwao kama ya harusi na shughuli nyingine za kifamilia na sio michango
ya miradi ya kimaendeleo ya serikali .
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa alisema zipo taarifa katika baadhi ya
vyombo vya habari ambavyo vimeripoti juu ya kuwepo kwa taarifa kutoka
mmoja kati ya mkoa ambapo mabalozi wa nyumba kumi wamekuwa wakitaka
kulipwa fedha kiasi cha shilingi 500 kutoka kwa wananchi wanaofika
kuwahamasisha kushiriki sensa.
Kwani alisema kuwa mkoa wa Iringa
umefanya uhamasishaji wa kutosha juu ya sensa na bado unaendelea kufanya na
hivyo rai ya ofisi yake ni kuwataka wananchi wote kushiriki katika zoezi
hilo bila kuogopa jambo lolote kwani taarifa zote za sensa ni siri na
zinachukuliwa kwa ajili ya matumizi ya sensa pekee.
Aidha alisema kuwa wale wote watakaofanya kazi ya sensa watakuwa na
vitambulisho kamili na mavazi maalum kwa ajili ya shughuli hiyo .
Wakati huo huo mkuu huyo wa mkoa aliwataka wananchi wa mkoa wa
Iringa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la sensa huku akiwataka
watu wenye ulemavu kutofichwa kwani wanahaki ya kuhesabiwa pia
No comments:
Post a Comment