August 7, 2012

MFUNGO MWEMA NA DUA NJEMA


Asalaam Alaykum Warahmatu llahi Wabarakatu

Ama Baada ya Salamu naomba Toa Shukran zangu za Dhati kwako Kaka na Timu Nzima ya Blog hii ya Jamii Japo Nimechelewa kuwatakia Kheri ya Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani Wadau wote pamoja na Timu yako Naomba Pokea Salamu zangu na Tunamuomba M/Mungu azipokee Funga Zetu na Dua zetu kwa Ujumla.

Naomba Nita barouk kidogo ( Tupate barka ) kwa Pamoja kwa kukumbushana Siku hii Muhimu katika Siku ambazo Ndio zimeufanya Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani kuwa Mwezi Mtukufu nayo Ni Siku ya LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO).

LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO) NI USIKU AMBAO UNAPATIKANA NDANI YA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI NDANI YA KUMI LA MWISHO MTUME (S.A.W) LILIPOKUWA LIKIINGIA KUMI LA MWISHO ALIKUWA AKIZIDISHA IBADA KWA SANA NA KUWA AMSHA WATU WAKE ( ALHAL BAYTI ) KWA AJILI YA KUFANYA IBADA ZAIDI KATIKA KUMI HILO. LAYLATU QADIR SI MWEZI 27 TU ILA WENGI WA WANACHUONI WAMEJITAHIDI KUWA HIYO NDIO SIKU YA LAYLATUL QADIR SIKU HII INAPATIKANA NDANI YA MWEZI 21 , 23 , 25 , 27 , 29 , NI JUU YETU NDUGU ZANGU KUITAFUTA SIKU HII KWA KUFANYA
IBADA KWA WINGI NDANI YA KUMI LA MWISHO ILI M/MUNGU ATUWEZESHE KUIDIRIKI SIKU AMBAYO UBORA WAKE NI ZAIDI YA MIEZI 1000 NA HUSHUKA MALAIKA NDANI YA SIKU HIYO KWA IDHINI YA M/MUNGU SUBHANAHU WATAALAAH .


UTUFUKU WA SIKU HII NI UNAPATIKANA KWA MAMBO MENGINE YAFUATAYO 1.KUTEREMKA KWA QUR AN ( MUNGOZO WA MUISLAM)


2.KUSHUKA KWA MALAIKA KWA IDHINI YA MOLA MTUKUFU NA MAILAIKA JIBRIL.


3.IBADA YA SIKU HII UBORA WAKE NI ZAIDI YA MIEZI 1000.

NI JUU YETU KUHAMASISHANA NAKUKUMBUSHANA KUWA SIKU HII NI SIKU MOJA NA MUHIMU SANA KUITAFUTA KWA KUKAA ITKAFU NA KUZIDISHA IBADA
ILI KUPATA KUMUOMBA MUNGU NA KULIOMBEA TAIFA LETU NCHI YETU YA TANZANIA MUNGU KUIPA BARKA.

SIKU HII MUNGU AKIKUBARIKI KUIDIRIKI DUA YA KUOMBA NI HII KWA MAELEKEZO YA MAMA AISHA
alimuliza Mtume Jee? tukiidiriki LAYLATUL QADIR (USIKU WA CHEO) tufanye nini ? Mtume akajibu kithrisha kusema NASH-HADU ANLAA ILAAHA ILLA ALLAHU NASTAGHFIRULLAH NAS'ALUKAL JANNATA ILAAHI WANAUDHUBIKA MINA NNAAR ALLAHUMA INNAKA AFUWUN TUHIBUL AFWAA FA'AFUANNAA YAA KARIYMAL AFWU ". Maana yake TUSHUHUDILIA HAKUNA M/MUNGU ISIPOKUWA WEWE ALLAH , TUNAKUTAKA MSAMAHA , TUNAKUOMBA PEPO YAKO NA TUNAJILINDA KWAKO KUTOKANA NA MOTO EWE M/MUNGU.
EWE M/MUNGU KWAKO NDIO KWENYE MSAMAHA WA KWELI UNAPENDA KUSAMEHE , TUSAMEHE WAJA WAKO EWE M/MUNGU WENYE SIFA YA UKARIMU ". Kama alivyosema Mtume

MUNGU NDIYE MJUZI WA HII SIKU LAKINI INAPATIKANA NDANI YA KUMI LA MWISHO LA RAMADHANI.

Nakushukuru sana Kaka wewe na Timu yako Mungu awabariki kwa ku - Post Ukumbusho huu Nawatakia kazi Njema.

Kwa Kumbusho zaidi utanipata katika Facebook kwa Id Name : Kijana wa Kiislam Dsm
au Twitter : Kijana wa Kiislam

Ghalib N Monero.
Al- Azhar University
Cairo Misri

No comments: