Mwenyekiti wa kamati ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas akipokea cheti toka kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dkt Emmanuel Nchimbi (kulia) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo.
Hakika kama ni msimamo wa wanahabari mkoa wa Iringa kutoshirikiana na jeshi la polisi katika kuripoti matukio mbali mbali ya wiki ya nenda kwa usalama iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Samora mjini Iringa ,umeyumbishwa kweli kweli na vituo vya radio ama kumekuwepo na lugha gongana kwa wanahabari hao.
Siku mbili zimepita toka kituo cha radio Counrty Fm Iringa kiliposhambuliwa kwa kurusha matangazo ya moja kwa moja kutoka uwanja wa samora katika maadhimisho hayo kwa madia kuwa kilikiuka makubaliano ya pamoja yaliyowekwa na wanahabari katika kususia kushirikiana na jeshi la polisi na hata kutuhumiwa kuhongwa pesa ili kusaliti msimamo huo jambo ambalo Bw Temy Mahondo aliweza kutolea ufafanuzi kuwa wao walipokea fedha kwa ajili ya matangazo sio vinginevyo.
Leo tena tunashuhudia kituo cha radio Ebony Fm cha Iringa pia kinaingia katika kundi kama hilo la kusaliti mshikamano wa wanahabari Iringa kwa kurusha tena kwa uzito zaidi maadhimisho hayo hali ambayo imenifanya kama kiongozi wa IPC kupigiwa simu nyingi sana na wanahabari wakihoji juu ya radio Ebony Fm kusaliti pia msimamo wetu .
Nasema kwa bahati mbaya wakati napigiwa simu kuwa sikiliza online radio Ebony kweli nilikuwa mbali na Laptop yangu sikuweza kusikiliza ila kama ni kweli radio Ebony Fm wamerusha maadhimisho hayo nategemea ushirikiano walioonyesha siku Radio Counrty Fm ilivyotangaza maadhimisho hayo ndivyo ambayo leo watanipigia simu mimi ama katibu wangu Frank Leonard aliyeko huko Ili kuelezea suala hilo .
Katika hili lazima utolewe ufafanuzi kwa wanahabari wote kama tumeamua kusitisha msimamo na kuamua kuendelea kufanya kazi na jeshi la polisi ni lazima ijulikane vinginevyo hakukuwa na haja ya kuweka msimamo kufuatia kifo cha Daudi Mwangosi .
Upo usemi unaosema kuwa mdogo akichukua mboga nyingi zaidi hulalamikiwa na hata kuadhibiwa kwa kudaiwa kukomba mboga na mkubwa akifanya hivyo kwake ni kawaida nachotaka kusema hapa radio zote ni sawa na vyombo vyote ni sawa lazima msimamo uwe kwa vyombo vyote na wanahabari wote .
Naendelea kuwasiliana na katibu wangu ili kutoa tamko katika hilo kupitia wanahabari wote bila kujali ni mwanachama ama si mwanachama wa IPC kiukweli nimevunjika moyo kabisa kwa yanayoendelea kutokea Iringa
Huu ni mtazamo wangu na si msimamo wa IPC naomba ieleweke hivyo

3 comments:
Ninasikitika sana kuona Wanahabari mpo katika Mgomo!
Sisi wananchi tilitegemea kupata elimu ya usalama barabarani kupitia vyombo vya habari, lakini mgomo wenu umesababisha tukose habari muhimu. Tunashukuru sana Blogs ambazo zilikuwepo Iringa kwaajili ya kuhabarisha umma juu ya Maadhimisho hayo. Hivi niwaulize Waandishi wa Iringa inapotok ajali ni polisi wangapi hufa au ni sisi wananchi? Wananchi tupo mbioni na sisi kugomea taarifa zenu hasagazeti.
Nawapongez walio ripoti tukio
kweli pesa kitu kibaya sana hata Yuda alimsaliti yesu, kwa hili sina imani tena na hao wanaojiita watangazaji.
Msipumbazwe na wanachokifanya hao jamaa zetu wa FM Radios za hapo Iringa!Endeleeni na msimamo wenu.Siku ikifika ya kusitisha mgomo,basi,mtalitolea tamko,na ulimwengu utawaelewa nini mlichokusudia kufanya!Asiye na akili timamu tu ndiye atakayeshindwa kuelewa ujumbe wenu ulikuwa na maana gani katika jamii!Viva IPC!
Post a Comment